Heri ya Pasaka: burudika na hadithi hii ya kutunga ya Jasusi iitwayo "Upendo wa Pasaka: Hadithi ya Emmanuel".
1. Ajali ya moto kabla ya Pasaka
Katika Jiji la London, nchini Uingereza, mbali na nyumbani kwao Tanzania, aliishi Emmanuel Mkono. Kijana mwenye nguvu, mwenye tabasamu na macho yaliyojaa ndoto, Emmanuel alikuwa mbali na familia yake akitafuta maisha mazuri zaidi. Alikuwa akifanya kazi mbili, kama mlinzi kwenye supamaketi na mpishi kwenye mgahawa mmoja wa…