#JinsiYaKuwaMtuBora: Jiulize "Mimi ni nani?" Hapana sio jina lako nani bali wewe kama mtu ni nani hasa? Majibu utayopata yatakushangaza
Ukiulizwa “wewe ni nani” jawabu la haraka litakuwa “mie ni flani.” Na hilo ni jibu sahihi kwa sababu muuliza swali alipaswa kufafanua kuwa anachouliza sio jina lako bali wewe kama mtu ni nani hasa?
Kwahiyo kabla ya kwenda mbali, chukua sekunde au hata dakika kadhaa kujiuliza swali hili “mimi ni nani?”
Japo kuna namna nyingi za kujibu swali hilo, kwa mfan…