Kozi ya Wiki Nane ya TAHAJUDI (meditation): Wiki ya Tatu - Jinsi ya Kukabilina na Hasira
Karibu katika kozi hii ya wiki nane ya TAHAJUDI (meditation). Hii ni nyenzo muhimu sana ya kukabiliana na changamoto kama vile msongo wa mawazo, kukata tamaa, kusikia uchungu, kuwa na hasira, wasiwasi, na hisia kama hizo.
Ili uweze kuimudu kozi hii na iwe na faida kwako ni muhimu kutokosa hata somo moja tangu kozi ilipoanza Novemba Mosi kwa wiki zote nane mfululizo.
Kila somo linaambatana na video yenye maelezo rahisi kwa lugha ya Kiswahili.
Karibu sana, na ikikupendeza, mkaribishe na mwenzio